MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Elikaeli Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi kwa kuugua ghafla usiku wa kuamkia leo na kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema, “Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC, madaktari walilazimika kumwekea mashine ya Oksijeni ili kuweka sawa afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: