Lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta ya petroli likitokea jijini Dar-es-Salaam kuelekea nchini Malawi limeteketea kwa moto leo katika eneo la Stamiko wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Jitihada za kuzima moto huo zinafanywa na kikozi cha zima mato na uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi na wananchi huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Mpaka sasa hakuna mamlaka yoyote ambayo imezungumzia tukio hilo, pia hakuna kifo wala majeruhi aliyeripotiwa kutokana na tukio hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: