Wimbi la Viongozi kutoka CHADEMA na kuhamia CCM linaendelea jijini Arusha ambapo licha ya madiwani wanaojiuzulu kila kukicha,Leo Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Arusha Gabriel Kivuyo amekihama chama hicho na kuamia CCM.
Akitangaza kujivua Uanachama huo na nyadhifa  zote alizo kuwa nazo ndani ya Chadema amesema ameamua kwa moyo wake mkunjufu ppkumuunga mkono Mh Rais magufuli katika kulijenga Taifa na kusimamia Rarisilimali za nchi hivyo hana sababu ya kubaki CHADEMA  wakati yote waliyokuwa wanayaamini sasa yanatelekezwa na CCM hivyo ameamua kujiunga na Ccm

Katibu huyo amepokelewa na Katibu wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg. Mussa Matoroka na   Katibu mwenezi wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.Abrahamu Mollel  pamoja na Katibu Hamasa wa Vijana Mkoa wa Arusha Ndg. Omary Lumato
Share To:

msumbanews

Post A Comment: