Zaidi ya ekari tatu za bangi zimeteketezwa kwenye msitu wa hifadhi ya Maisome iliyopo katika kisiwa cha Maisome Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .
Kwa mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Alan Mhina, bangi hiyo ilikuwa imelimwa kwenye sehemu ya msitu huo wenye ukubwa wa hekta 12,800, na kwamba, iliteketezwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya katika operesheni maalum ya kukomesha kilimo cha zao hilo haramu.
Kwa upande wake, Meneja Wakala wa Misitu Tanzania, TSF, Wilaya ya Sengerema, Bw. Urio Jeremiah, amesema, operesheni hiyo pia imelenga kukomesha shughuli nyingine za kibinadamu zinazotishia uhai wa hifadhi hiyo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: