Kikosi cha Yanga jana kilitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Botswana, Sylvester Ambokile, kwenye kambi waliyoweka mjini Gaborone.

Balozi huyo alienda kuitembelea Yanga ambayo inawakilisha Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kuweza kuzungumza machache na wachezaji, pamoja na viongozi wa timu hiyo.

Ambokile alipata fursa ya kukitembelea kikosi hicho kikiwa kinasubiri mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, utakayopigwa Jumamosi ya wiki hii.

Mbali na kutoa mawaidha kadhaa kwa wachezaji, Ambokile alipata wasaa wa kujumuika nao pamoja kula chakula cha jioni.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: