Wakristo
kote nchini wametakiwa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2019 wa
madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa na viongozi wa vitongoji kwa
kumchagua mtu asiyewafanya waishi kwa kuogopaogopa.
Kauli
hiyo imetolewa jana Machi 30 na Mhashamu Askofu Evarist Chengula
alipokuwa akiongoza ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika
kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Fatma lililopo Mwanjelwa mjini Mbeya.
Akihutubia
katika ibada hiyo Mhashamu Chengula alisema ujumbe uliotolewa na
maaskofu siku kadhaa zilizopita ulikuwa haumlengi mtu fulani bali
uliwalenga wanafiki wanaodai ni Wakristo lakini hawana imani ya Kikristo
ili waweze kubadilika na kuwa watu wema.
“Ujumbe wa mwaka huu tunasema hakuna maana kusikiliza kila kitu tu, badala yake tufikiri kabla ya kutenda.
“Imekuwa
kawaida kila baada ya kumalizika uchaguzi mkuu tunaanza kulaumiana,
Wakristo wote katika jumuiya zenu ndogo ndogo nchi nzima muanze
kujipanga mnataka mtu wa aina gani, angalieni ana tabia gani na si
anatoka chama fulani,” alisema Mhashamu Chengula. Amewataka wanaparokia kukaa na maaskofu na kujadili.
“Msipofanya hivyo mtarudi kule kule kwa kulaumiana. Chagueni kwa kuzingatia kila mmoja atendewe haki, apate haki na amani.” Alisema na kuongeza;
“Kila
baada ya uchaguzi wanakimbizana kama sungura na mbwa maana hatuchagui
anayetusaidia sisi, tunachagua chama fulani kituongoze na kitutetee
badala ya kufikiri kuchagua atakayetuongoza kwa amani.”
Aliongoza: “Haina
maana kutuchagulia watu fulani ambao tukiwachagua wanatuongoza kwa
woga, hawa hawajajiweka wenyewe ni mimi na wewe tumewaweka, tusichague
watu wenye roho ya ubinafsi.”
Alisema
ujumbe huo ni kwa wote, ili waanze kujiandaa kwa sababu unafika
uchaguzi wa mwaka 2019 wachague kwa kuangalia hali halisi.
“Kila
mmoja akasimulie hili anapokwenda kwa sababu ni vita ya wote, kila
mmoja awe makini Tanzania iwe na upendo na mshikamano kati yetu.
“Kila anayekuja kubusu msalaba huu tulioulaza hapo mbele amueleze Yesu nataka Tanzania yenye upendo,” alisema Mhashamu Askofu Chengula.
Post A Comment: