Shirika
la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)
limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa
wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza.
Msaada
huo umetolewa Jumanne Machi 27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold
Crest Hotel jijini Mwanza wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika
mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kupanga mipango na
mikakati ya kupambana na VVU na Ukimwi.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mashine hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mashine hizo ni kwa ajili ya vituo
vya afya vya Katunguru na Kabila vilivyopo wilaya ya Sengerema,
hospitali ya Ngudu iliyopo wilayani Kwimba na zahanati ya Kirumba na
kituo cha afya cha Buzuruga vilivyopo wilayani Ilemela.
Dk.
Sekela alisema mashine hizo tano zenye thamani ya shilingi milioni 6.8
zitatumika kutolea tiba mgando kwa akina mama wanaokutwa na dalili za
mwanzo za kansa ya uzazi. “Mbali na shirika letu kuendelea kuboresha
huduma za kinga na matunzo pia tunatoa huduma ya uchunguzi wa dalili
saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama”,alieleza.
Alisema
huduma hiyo hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika
mkoa wa Mwanza. Dk. Sekela alisema shirika hilo mpaka sasa limetoa
msaada wa ‘cryotherapy machines’ 17 katika mikoa sita ambayo ni
Mwanza,Shinyanga,Tanga,Geita,Simiyu na Mara zote zikiwa na thamani ya
jumla ya shilingi milioni 115.6.
Dk.
Sekela pia alikabidhi kompyuta 18 zitakazotumika kuhifadhi takwimu za
wateja wa CTC katika vituo vya afya husika na kusaidia upatikanaji wa
taarifa kwa haraka na kwa usahihi Zaidi mkoani Mwanza. “Tangu tuanze
mradi wa Boresha, tutakuwa tumetoa jumla ya kompyuta 82 kwa mkoa wa
Mwanza ambazo zinatumika kutunza taarifa za watu wenye VVU na
Ukimwi”,alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya wilaya zilizopokea mashine hizo,Mkuu wa wilaya ya
Sengerema Emmanuel Kipole alilishukuru shirika la AGPAHI kwa kutoa
msaada huo na kwamba watatumia vifaa vilivyotolewa kwa malengo
yaliyokusudiwa. Awali akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, John Mongella aliwataka wadau wote kuungana na kushirikiana ili
kuhakikisha kuwa maambukizi ya VVU mkoa huo ambayo sasa ni asilimia 7.2
yanapungua.
AGPAHI
ni shirika la Kitanzania linalofanya kazi kwa kushirikiana na serikali
ya Tanzania kutoa huduma za afya hususani watu wanaoishi na Maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi kwa fadhili wa Watu wa Marekani kupitia
Centres for Disease Control (CDC).
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza katika kikao cha wadau
wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kabla ya
makabidhiano ya kompyuta na mashine tano za kuchunguza saratani ya
shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’.- Picha zote na
Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea namna
shirika hilo linavyotoa huduma ya kuwapima saratani ya shingo ya kizazi
kwa wanawake.
Dk. Sekela akizungumza na wadau wa afya mkoani Mwanza.
Maboksi
yenye kompyuta na mashine za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi
kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ zilizotolewa na shirika la AGPAHI
kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Mwanza.
Kulia
ni Dk. Mwakyusa akiwa ameshikilia moja ya mashine inayotumika kuchunguza
saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’.
Dk. Sekela akizungumza ukumbini.
Katikati
ni Dk. Sekela Mwakyusa akikabidhi mashine kwa Mkuu wa mkoa wa
Mwanza,John Mongella (wa pili kushoto) na viongozi wa wilaya ya
Sengerema.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha akipokea cryotherapy machine.
Mkuu
wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole akitoa neno la shukrani baada ya
makabidhiano ya mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi
kwa wanawake na kompyuta 18 zilizotolewa na shirika la AGPAHI.
Post A Comment: