Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP  WILBROD MUTAFUNGWA  leo ametembelea  kijiji cha  Ipole wilaya Sikonge  ambako Magari zaidi ya 30 yalikwama kutokana na kukatika kwa barabara  ya Tabora - Mpanda kulikosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Kamanda  Mutafungwa ameongea na wasafiri waliokwama hapo kwa muda wa siku mbili na kuwahakikishia kuwa barabara hiyo itatengemaa kwa muda mfupi na wataendelea na safari yao.kutokana na jitihada kubwa zinazoendelea kufanyika kwa ushirikiano na wakala wa Barabara TANROAD

Abiria hao wametoa shukrani zao kwa Jeshi la Polisi kwa namna walivyoshirikiana nao kwa kuhakikisha  ulinzi na usalama umekuwepo kwa muda wote katika eneo hilo.

Zoezi la urekebishaji wa barabara hiyo linaendelea vizuri huku baadhi ya magari ya abiria yakiwa yameanza safari zake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: