Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mombasa kwenda Nairobi nchini Kenya, wamelichoma basi walilokuwa wakisafiria katika eneo la Tajmali huko Embakasi.
Chanzo cha abiria hao kufanya hivyo kimeelezwa kuwa ni hasira walizokuwa nazo baada ya dereva kulazimisha kutumia njia ambayo imeathirika na mafuriko, na kuhofia kukaa njiani kwa muda mrefu kutokana na foleni.
Abiria hao walikuwa wakimtaka dereva kutumia njia ya kupitia Outering kwenda Nairobi, badala ya barabara ya Mombasa ambayo dereva alikuwa akisisitiza kuitumia.
Baada ya mvutano wa hapa na pale ndipo abiria hao waliposhikwa na hasira na kuamua kulichoma moto basi hilo na kisha wote kukimbia, na dereva naye kuamua kukimbia eneo la tukio.
Source
Ghetto Radio Kenya
Basi lililochomwa moto na abiria
Share To:

msumbanews

Post A Comment: