0
5
Serikali nchini Zimbabwe inatarajia kujenga sanamu kubwa ya Bob Marley na kuiweka katika nchi hiyo, kama ishara ya kumuenzi mwanamuziki huyo nguli wa reggae duniani.
Nchi hiyo ilipata bahati ya kutembelewa na Bob Marley ambaye alikuwa na hamasa kubwa kwenye harakati za ukombozi barani Afrika.
Serikali ya Zimbabwe imesema kuwa sanamu hiyo itatengenezwa na wataalam kutoka Afrika Kusini, na itakuwa ni kama alama kubwa kwa wana Zimbabwe wakikumbuka mchango wake kwenye Uhuru wa chi hiyo.
Bob Marley alienda kufanya tamasha nchini Zimbabwe siku ya uhuru wa nchi hiyo, na kuimba wimbo maalum unaohusu uhuru wa nchi hiyo maarufu kama ‘Zimbabwe’, ulioleta hamasa kubwa kwa nchi za Afrika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: