Klabu ya Yanga imetinga robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Majimaji FC, mchezo uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa pande zote mbili huku Majimaji wakiongoza kumiliki mpira, Nyavu za Majimaji ndio zilianza kuchezewa na Yanga kupitia kwa Pius Buswita katika dakika ya 40.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa pande zote mbili huku Majimaji wakiongoza kumiliki mpira, Nyavu za Majimaji ndio zilianza kuchezewa na Yanga kupitia kwa Pius Buswita katika dakika ya 40.
Katika kipindi cha pilidakika ya 52, Emmanuel Martin alifunga Yanga goli la pili kwa njia ya kichwa, akiunganisha krosi nzuri ya Hassan Kessy, na kufanya matokeo yawe mabao mawili kwa Yanga na sufuri kwa Majimaji.
Goli la kufutia machozi la Majimaji lilifungwa kunako dakika ya 61 ya mchezo na Jaffar Mohammed na kufanya ubao wa matokeo kubadilika kuwa 2-1 hadi mchezo huo unamalizika.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo inakuwa ni timu ya tano kufuzu.
Post A Comment: