Waziri Ndalichako ameyasema hayo hii leo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza kuwa anategemea kuona matokeo chanya kutoka kwenye bodi hiyo kwa kuwa wote walioteuliwa wamebobea katika masuala mbalimbali yanayohusu Elimu.
Dk. Katunzi amesema kuwa wamepokea kwa mikono miwili uteuzi huo na kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu Kati ya bodi na uongozi wa ADEM.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu Dk. Joseph Masanja amesema bodi hiyo itaishauri ADEM katika masuala mbalimbali ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
Bodi hiyo ambayo imezinduliwa leo itatekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka Mitatu.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
3/2/2018
Post A Comment: