Serikali ya Tanzania imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa Maktaba ya kisasa pamoja na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa  kujenga Maktaba ya kisasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 na kihifadhi vitabu 800,000 kwa mara moja.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua hatua za ujenzi unavyoendelea Chuoni hapo jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ppppProfesa Joyce Ndalichako amesema Serikali ya China inatambua vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano hivyo wameahidi kuisaidia Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vipaumbele vilivyowekwa ikiwemo  Elimu inatimiza malengo yaliyokusudiwa.

Waziri Ndalichako amesema Maktaba hiyo ya kisasa na kubwa barani Afrika pia inajumuisha jengo la Taasisi ya Confucius ambayo imekuwa ikifundisha lugha na tamaduni za kichina kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam  na watanzania, jengo hilo pia linakumbi za Mubashara, pia vyumba vyenye kompyuta za kisasa zenye programu maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya China hapa nchini Wang Ke amemhakikishia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzani katika maeneo mbali ikiwemo Sekta ya Elimu.


Ujenzi wa Maktaba hiyo unaotarajiwa kukamilika Julai 2018 utagharimu  dola za kimarekani 41,280, 000.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

9/2/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: