Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amezindua Jengo la Mama na Mtoto Hospital ya Amana lililojengwa kwa jitiada binafsi za RC Makonda kutafuta wafadhili wa kampuni ya Amsons Group iliyoridhia kujenga jengo hilo pasipo kutumia fedha ya Serikali.
Ujenzi wa jengo hilo lenye thamani ya Billion 1.2 ni matokeo ya RC Makonda kuona mateso na uchungu waliokuwa wakipata kinamama waliokuwa wakijifungua kwenye Jengo Dogo na Chakavu "kibanda" lililojengwa Miaka 60 iliyopita hali iliyokuwa ikisababisha kulala kitanda kimoja watu watatu hadi wanne "mzungu wa nne" na wakati mwingine wagonjwa kuja na godoro au kanga nyumbani ili aweze kuweka chini alale.
Kwa sasa kinamama wanafurahia maisha kwa kutumia jengo la kisasa la gorofa mbili na ground floor ambapo ndani yake kuna wodi za kisasa, vyumba vya upasuaji, Mahabara, vitanda vya kisasa 150 vyenye neti na makabati yake, feni,mapokezi,sehemu ya mapumziko na madirisha ya Vioo yanayoruhusu mwnga na hewa ya kutosha.
RC Makonda amesema awali kinamama wanaojifungua walilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda kutokana na kukosekana kwa jengo la kutosheleza mahitaji hivyo jengo litamaliza changamoto hiyo.
Aidha Makonda amesema uwepo wa jengo hilo utasaidia kupunguza idadi ya vifo vya Mama na Mtoto waliokuwa wakipoteza maisha kwa kujifungua kwenye mazingira yasiyo rafiki.
Aidha ameshukuru kampuni za Amsons Group kwa kufanikisha ujenzi wa jengo hilo na kueleza kuwa kwa sasa wanajenga jengo Kama hilo Hospital ya Mwananyamala kisha Temeke ambapo pia kuwapongeza watumishi wote wa sekta ya afya kwa kutoa huduma bora na kupunguza malalamiko ya wananchi.
Nao viongozi walioshiriki uzinduzi huo akiwemo Naibu waziri wa Afya, Wakuu wa wilaya, Wabunge, Wakuu wa idara, madiwani,wenyeviti wa mitaa na wananchi wamemsifu RC Makonda kwa kuleta ukombozi kwenye Mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi ya kinamama wameeleza kuwa jengo hilo ni zuri na lakisasa kwakuwa lina vitu vyote muhimu ambapo baadhi yao wamesema hawatamani hata kuruhusiwa kurudi nyumbani ambapo wamemshukuru RC Makonda kwa kuona kilio chao cha muda mrefu na kukipatia ufumbuzi.
HONGERA RC MAKONDA KWA KUTIMIZA NDOTO ZA RAIS MAGUFULI.
Post A Comment: