Waziri Wa mambo ya ndani ya nchi Dr.Mwigulu Nchemba amewahakikishia usalama wananchi wote ambao majimbo yao na kata zao zinafanya uchaguzi marudio na kuwataka kujitokeza Kwa wingi kupiga kura pasipo kuhofia usalama wao.
Dr Nchemba amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutokumwonea haya kumchukulia hatua Kali mtu yeyote atakayeshiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani katika kampeni zinazoendelea au katika uchaguzi utakao fanyika february 17.
Akizungumza leo katika kampeni ya kumnadi mgombea udiwani kata ya Madanga ndugu Athumani Tunutu.Dk mwigulu aliwataka wananchi kukiamini chamacha mapinduzi CCM Kwa kumchagua Tunutu ili awaletee maendekeo kwani ilani inayotekelezwa ni ya chama cha mapinduzi hivyo ni rahisi kwa wao kuoata maendeleo kuliko kuchagua upinzani ambao wao mda wote ni kupinga maendeleo.
Post A Comment: