Wanafunzi saba wa chuo kikuu cha waislamu Morogoro wamekatisha masomo yao kwa kufukuzwa chuo hapo kwa sababu mbalimbali, sita kati yao wamefukuzwa mojakwa moja wasirudi chuo  na mmoja amefukuzwa kwa muda wa muhula mmoja.

Akizungumza jana mara baada ya swala ya ijumaa iliyofanyika chuoni hapo, mwenyekiti wa kamati ya Nidhamu chuoni hapo Sheikhe Abdul Kassim Jiba alisema wanafunzi hao  wamefukuzwa kwa makosa tofauti ikiwemo ugonvi lakini wengi wao wamefukuzwa kwa sababu ya mahusiano (Mapenzi).

Pia shekhe jiba alitumia muda huo kuwaasa wanafunzi chuoni hapo kufuata sheria za chuo ikiwa pamoja na kutojihusisha na masuala ya mapenzi ,pia hairuhusiwi kutembea au kukaa wawili mwanamke na mwanaume isipokuwa awepo mtu wa tatu.

Kwa mujibu wa sheria za chuo hicho ni kosa kwa mwanafunzi kuwa na mahusiano ya kimapenzi ukiwa chuoni au likizo nyumbani isipokuwa kwa mke au mume. kama umeoa au kuolewa unatakiwa kuwasilisha cheti cha ndoa kwa uongozi wa chuo ili kutambua uhusiano wako.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: