Mara baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya timu ya Lipuli FC mchezaji wa klabu ya Yanga,Kelvin Yondani amekabidhiwa kitita cha fedha shilingi milioni moja na mwenye kiti wa group la wana jangwani hao, Hamad Islam.
Yondani amekabidhiwa fedha hizo ikiwa ni motisha kutokana matokeo mazuri kwenye mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Lipuli FC huku group hilo linalo jumuisha wanachama wa Yanga SC kuahidi kuwapatia Zaidi wachezaji kwenye kila mechi ambayo timu hiyo itapata ushindi.
Juma mosi ya wikiendi hii iliyopita mabingwa wa kihistoria Yanga SC walishuka katika duimba la Samora na kucheza na wenyeji wao Lipuli ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kufunguliwa kwa mzunguko huu wa pili na kufanikiwa kuchomoza na ushindi huo mujarabu wa mabao 2 – 0.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa muhumu kwa pande zote mbili Yanga SC ilipata mabao yake kupitia kwa kiungo wake wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi dakika ya 19 na la pili likifungwa na Buswita dakika ya 55. Ushindi uliyoifanya Yanga SC ifikishe pointi 31 baada ya kucheza mechi 16
Post A Comment: