Mjema amekabidhi vitambulisho hivyo leo Februari 6, 2018 na kubainisha kuwa vitaendelea kutolewa kwa wafanyabiashara hao maarufu kama wamachinga.
“Hakuna mmachinga katika soko hili atakayeachwa. Vitambulisho hivi vitawasaidia kupata hati za kusafiria na mtaweza kwenda nje ya nchi kununua bidhaa na kuachana na utumwa wa kutumwa na wafanyabiashara wakubwa,” amesema Mjema,
"Tunataka wamachinga wa mkoa wa Dar es Salaam wawe mfano wa mikoa yote, leo tunawakabidhi vitambulisho wamachinga 1,984 na baadaye vitaendelea kutolewa kwa wote hakuna atakayeachwa.”
Ofisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) Wilaya ya Ilala, Ubba Ponda amesema wamachinga waliosajiliwa walikuwa 3,115, kati yao 1,984 vitambulisho vyao vimekamilika na 1,131 bado havijakamilika.
Post A Comment: