Tangu wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kuanza kufanya kazi mmoja mmoja, Beka Flavour amekuwa akifanya vizuri kwa kiasi kikubwa.
Beka ameweza kutoa ngoma kama Libebe, Sikinai, Umenimaliza, Sarafina na sasa anatamba na ngoma ‘Kibeniten’ ambayo ni mpya.
Katika video yake mpya ‘Kibenten’ mpenzi wake ndiye amecheza kama video queen, na hii ni kutokana na aliyetarajiwa kufanya hivyo kutofika location siku husika.
Beka si msanii wa kwanza kufanya hivyo, kuna Diamond alifanya hivyo kwa Zari katika video ya Utanipenda, Harmonize na Wolper katika video ya Niambie, Barnaba na Mama Steve katika video ya Wahalade, Nuh Mziwanda na Shilole katika video ya Msondo Ngoma.
Beka si msanii wa kwanza kufanya hivyo, kuna Diamond alifanya hivyo kwa Zari katika video ya Utanipenda, Harmonize na Wolper katika video ya Niambie, Barnaba na Mama Steve katika video ya Wahalade, Nuh Mziwanda na Shilole katika video ya Msondo Ngoma.
Hata hivyo wasanii hao niliowataja hapo juu kwa sasa mahusiano yao yanaripotiwa kuvunjika ila kuna ambao walifanya hivyo na hadi sasa wapo katika mahusiano yao;
Mabeste
Alimshirikisha mke wake ‘Lisa’ kwenye wimbo wake ‘Usiwe bubu’, pia mkewe aliwahi kuwa meneja wa kusimamia kazi zake.
Jux
Mpenzi wake Vanessa Mdee alionekana kwenye video ya wimbo wa Sisikii uliotoka mwaka 2014, hii ilikuwa ni kabla ya kuja kuachia wimbo wao wa pamoja uitwao Juu.
Rayvanny
Hapo awali kulikuwa na drama za hapa na pale kuwa Rayvanny ameachana na Baby Mama wake, Fahyma lakini hilo lilikuja kuzimwa mara baada ya Fahyma kuonekana katika video ya Rayvanny ‘Safari’ aliyomshirikisha Nikki wa Pili.
Hivyo basi Beka amekuja kuongeza idadi ya wasanii waliowatumia wapenzi wao katika video za ngoma zao, hata hivyo baadhi ya wasanii hawa hawapendi wapenzi wao kutokea katika video za wasanii wengine.
Post A Comment: