Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza Gypsum cha ST, GOBAIN LODHIA kilichopo Kikatiti ,wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Sailesh Pandit ametishia kukifunga kutokana na kupanda Marà dufu kwa gharama ya malighafi ya Makaa ya Mawe yanayotumika kiwandani hapo.
Aidha ameiomba serikali kuangalia uwezekano Wa kuwapunguzia gharama za bidhaa hiyo ili waweze kujiendesha kwa faida tofauti na sasa ambapo kiwanda hicho kinajiendesha kwa hasara.
Pandit ameyasema hayo jana jmosi feb 10 wakati akizungumza na wafanyakazi wake baada ya wafanyakazi hao kudai nyongeza ya mshahara.
Amesema kuwa awali serikali ilikuwa ikiwatoza asilimia 10 ya thamani ya mzigo Wa Makaa ya Mawe lakini ghafla ilipandisha na kufikia asilimia 25 jambo linalopelekea kupata hasara ya zaidi ya sh, milioni 30 kila mwezi.
Amesema kuwa iwapo serikali haitasikia kilio chake atalazimika kusitisha uzalishaji hadi hapo hali itakapokuwa nzuri.
Amewasihi wafanyakazi wake ambao ni zaidi ya 1000 kuwa wavumilivu wakati akifanya mawasiliano na serikali.
Post A Comment: