Vurugu kubwa zimeibuka katika Baraza la madiwani wa  Halmashauri ya Jiji la  Arusha  kufuatia madiwani wa Chadema kususia na kutoka nje ya ukumbi katika tukio la kuapishwa kwa madiwani wapya wawili wa waliochaguliwa kupitia chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo uliyo pita.


Tukio hilo limetokea mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha baada ya Mkurugenzi wa Jiji Athmani Kihamia kusoma agenda ya kuapishwa kwa madiwani hao ndipo madiwani wa chadema walitoka nje kupinga kuapishwa kwa madiwani hao wa chama cha mapinduzi na mara baada ya kutoka nje ya ukumbi ndipo walipi kutana na wafuasi wa chama cha mapinduzi ccm waliyokuwa nje ya ukumbi wa baraza ili kushuhudia kuapishwa kwa madiwani wa chama chao ndipo hapo vurugu zikaanza na wafuasi wa Ccm kuanza kuwazomea madiwani wa chadema.


Licha ya vurugu hizo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia alijaribu kutuliza vurugu hizo huku akiwataka madiwani waliotoka nje warudi ndani ya ukumbi ili kuendelea na kikao cha baraza lakini maombi yake kwa madiwani hao haikuwa na mafanikio na badara yake kelele za vurugu zikiendelea kulindima baina ya madiwani wa chadema na wanachama wa chama cha mapinduzi kitu kilichopelekea jeahi la polisi kuchukua nafasi yake kufika katika viunga vya Halmashauri ya jiji la Arusha ili kutuliza ghasia ndipo madiwani hao waliamua kurudi ndani ya ukumbi huku wafuasi wa ccm walipo ondoka katika maeneo ya viwanja vya Halmashauri ya jiji la Arusha.


Kwa upande wake Meya wajiji la Arusha Calist Lazaro ndiyo diwani pekee wa chama cha demokrasia na maendeleo Chandema hakuweza kutoka nje pamoja na Naibu Meya Viola Lazaro hawakuungana na madiwani wenzake wa chadema na kupelekea madiwani hao kurudi ukumbini huku wakiendelea kurumbana ndipo Meya alisimama na kuginga nyundo mezani ili kutuliza vurugu hizo lakini hazikuzaa matunda na badala yake vutugu zikaendelea na ndipo askari wa jiji walipo ingilia kati vurugu hizo zilizo dumu zaidi ya nusu saa.


Baada ya vurugu hizo kuisha wafuasi wa CCM waliondoka na Madiwani wao wawili ambao ni Fransis Mbise Diwani wa Kata ya Murriet na Gaudence  Lyimo wa Kata ya Kimandolu  huku wafuasi wa CCM wakishangilia mara baada ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Chrisanta  Chitanda akisaidiwa na  Mwanasheria wa Jiji hilo, Braison  Orcado kuwaapisha madiwani hao wa chama cha mapinduzi huku madiwani hao wakiondoka na wasiasi wao kuelekea ofisi za ccm ngazi ya wilaya na kuacha baraza likiendelea.



Baadhi ya madiwani wakiongea na Msumbanews Blog wakieleza sababu za vurugu hizo ni kupeleka ujumbe kwa serikali kuu kwamba hawajakubaliana na uchaguzi mdogo uliyopita kwamba haukuwa wa huru na wahaki na demokrasia haikutumika katika chaguzi hizo ndogo za madiwani kitu walicho eleza sio haki kwa watanzania na taifa huru kama tanzania.


Baada ya hali kuwa shwari na baraza kuanza Naibu Meya ,Viola Lazaro alitoa hoja kwa madiwani hao kuhamasisha wananchi kupima afya zao ikiwemo kusindikiza kinamama wajawazito kuhudhuria kliniki ili waweze kupima afya zao na kupunguza maambukizi ya virusi vya Vvu na ukimwi.


Mjada mwingine ulichukua nafasi kubwa katika baraza hilo la madiwani ni swala la maduka ya stend ndogo jiji la Arusha kutokufikia tamati licha ya mikataba mbali mbali kutolewa kwa baadhi ya vibanda huku majadiliano yakifanyika kwa viongozi ya wafanyabiashara na serikali lakini mgogoto huwa kutokupata ufumbuzi kitu ambacho madiwani walimtupia lawama Meya wa jiji la Arusha kuwa amewageuka na kudai kuwa maduka ya stend ndogo ya maslahi binafsi kwa baadhi ya viongozi.


Akichangia ajenda hiyo diwani wa kata ya Olasiti Mh Alex Marti, aliwataka madiwani wenzake kufikia hadhima.ya pamoja ya kuwaruhusu Meya na Mkurugenzi kusaini mikataba hiyo na kuwapatia wafanya biashara hao kitu ambacho kilikubaliwa na mkurugenzi kuahidi kulifanyia kazi kwa wakati na hayupo tayari kuyumbishwa tena juu ya mgogoro wa stend ndogo.


Kufuatia swala hilo kutokufika tamati kwa muda mrefu katika kufunga ajenda hiyo mkurugenzi wa jiji alisema kuwa kuna dalili zote za rushwa na kuwataka madiwani hao kuto chukua rushwa na kuwagombanisha wananchi na serikali huku tamati ya jambo hilo baraza imeamua kusaini mikataba upya kuanzia kesho na kuendelea ili kuwaacha wananchi kufanya biasha kwa mujibu wa sheria na kisha meya kuhairisha baraza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: