TAARIFA KUTOKA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI 06:02:2018
Leo Mh:mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Amefunguliwa kesi mahakama ya Wilaya Sekei ya kushambulio na kudhuru tukio linalodaiwa kutendwa mwaka mwaka 2014 kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa. Kesi hiyo iliyofunguliwa na aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Makiba Ndugu Naiman Ngugu.
Hata hivyo HAKIMU Jasmini amesema upelelezi haujakamilika tangu mwaka 2014 kesi itaendelea tar 06 /03/2018 .
Mhe Mbubge Nasari amepewa dhamana na kutakiwa awe na mdhamini mmoja kwa dhamana ya sh milioni 5
Mhe Nasari Mbunge amedhaminiwa na amesharudi Bungeni kuendelea vikao Vya bunge vinavyoendelea Dodoma.
Imetolewa na Katibu ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki
Julius Ayo
06:03:2018
Post A Comment: