Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani Mtwara imezifungia hoteil tatu pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi zaidi ya Sh bilioni 1.
Hotel zilizofungiwa ni Naff Beach, Naf blue na BNN wakati kituo cha mafuta kilichofungiwa pamoja na kituo cha mafuta kijulikanacho kwa jina la Mnarani Petrol Station.
Afisa mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian Byabato ameliambia gazeti la Dailynews kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.
“Ni madeni ambayo yametokana na ukaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma, kikubwa walipe kodi..tunafungia kwa mambo mbalimbali kama malimbukizo ya madeni ya muda mrefu, matumizi sahihi ya mashine za EFD katika kutoa na kudai risiti sahihi inayoakisi gharama halisi ya malipo na kutii sharia za kodi kama kutunza kumbukumbu,” amesema Byabato
Byabato ameongeza kuwa endapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
Share To:

msumbanews

Post A Comment: