Image result for kocha JULIO

Pamoja na juhudi kuu alizokuwa akizifanya, Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kurejea Ligi Kuu Bara.

Kikosi chake cha Dodoma FC kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African lakini timu inaendelea kubaki Ligi Daraja la Kwanza.

Hiyo inatokana na ushindi wa Biashara Mara dhidi ya Transit Camp ambao umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 30 na Alliance imefikisha pointi 28 baada ya kuitwanga JKT Oljoro.

Ushindi wa leo umeifanya Dodoma FC kufikisha pointi28 pia lakini wastani wake wa mabao ya kufunga na kufungwa ndiyo yanaibakisha Ligi Daraja la Kwanza
Share To:

Post A Comment: