Serikali imesema Tanzania inazidi kupaa zaidi kiuchuni barani Afrika baada ya kutajwa na ripoti ya Foresight Afrika iliyotolewa mwaka 2018.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya tano Africa huku nafasi nne za juu zikishikiliwa na Senegali, Ivory Coast, Ethiopia na Ghana.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii, Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas amesema serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikiimarika kiuchumi kila siku.
“Kwa mujibu wa ripoti ya FORESIGHT AFRICA iliyotolewa mwaka huu (2018) Tanzania ipo kwenye 5 bora ya nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi barani Afrika, Ghana ndio imeongoza orodha hiyo kama inavyoonesha,” alisema Abbas.
Katika hatua nyingne Abbas amesema Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza kwa utawala bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ikifuatiwa na majirani zetu Kenya na imekuwa ya 91 duniani.
Post A Comment: