Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkindi wa kusaini makubaliano ya kufanya kazi Pamoja kati ya Tanzania Horticulture Association Mboga (TAHA) na Taasisi ya Serikali inayofanya Ubia na wadau wa Maendeleo (PASS),Mkurugenzi Mtendaji  PASS  Nicomed  Bohay



Wakulima hapa Nchini wanatarajia kunufaika kwa kuwezeshwa kwa rasiliamili fedha ili kuweza kufanya kilimo cha kisasa na kukua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Akizungumza Wakati wa kusaini makubaliano ya kufanya kazi Pamoja kati ya Tanzania Horticulture Association Mboga (TAHA) na Taasisi ya Serikali inayofanya Ubia na wadau wa Maendeleo (PASS), Mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkindi amesema kuwa sekta ya Matunda na mboga mboga hapa nchini inakua kwa kasi kiasi cha kuajiri Vijana wengi kutokana na teknolojia za kiasasa.

Aidha amesema changamoto kubwa ni rasilimali  fedha ambayo kwa kiasi kikubwa imetatuliwa na PASS kwa kuwa taasisi za fedha zimekuwa zikishindwa kuwaamini wakulima kwa kuwapatia mitaji kwa kukosa thamana.

Mkindi amesema sasa wakulima watapata Mikopo kwa Udhamini wa PASS Hivyo kuwawezesha kupata maendeleo makubwa na kuondokana na uzalishaji wa kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji  PASS  Nicomed  Bohay-
Amesema lengo ni kuondoa umaskini  na kutoa Ajira kwa Wakulima hapa nchinui.

Aidha  amesema changamoto kubwa ambayo wakulima wamekuwa wakikosa mitaji na Amana kutokana na masharti magumu ambayo wamekuwa wakiwekewa na taasisi mbali mbali za fedha hapa nchini ambapo kupitia mpango huo Pass itawawezesha kukopa bila masharti magumu kama yalivyo .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: