Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha (CHADEMA) Elvis Mossy amefungukia matamko yanayotolewa ya kuhusu kupiga kura na kwenda nyumbani ambapo amesema kwamba matamko hayo yanakinzana kanuni ingawa ametaka haki itendeke kwani wananchi wake siyo watu wa vurugu

Akizungumza akiwa kata ya Engarenairobi huko Siha mkoani Kilimanjaro, Mossy amesema kwamba kanuni zinahitaji watu wajae mita 100 baada ya kupiga kura lakini kama haki itatendeka wananchi wa Siha hawatakuwa na haja ya kulinda kura.

"Hatuna vurugu sisi. Kama wanataka turudi majumbani tutaenda tu. sisi tunachotaka ni haki, akishinda Mollel atangazwe lakini nikishinda mimi nitangazwe. Ila Kailima anajua kwamba kanuni zimeweka wazi mpiga kura anapaswa kukaa mita kadhaa baada ya kupiga kura" Elvis

Akizungumzia changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza, Mossy amesema kwamba mawasiliano yamekuwa kikwazo kikubwa kwani fomu za kura zimekuwa chache katika moja ya kituo lakini Mkurugenzi hapokei simu ili kuweza kutatua changamoto hiyo.
"Mawasiliano ni changamoto ya kwanza, Mkurugenzi wetu wa hapa hapokei simu lakini nimemwambia Kailima ameahidi kutusaidia. kuna kituo kina fomu 60 na wakati zinahitajika kama 400

Mbali na hayo taarifa mbalimbali zinasema katika jimbo la Siha watu mbalimbali wamejitokeza kupiga kura huku eneo la Sanya Juu wazee wakionekana kuwa wengi kuliko vijana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: