Klabu ya Singida United inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara imetangaza kurejea uwanjani kwa mchezaji wake wa kimataifa wa Rwanda, Dany Usengimana kufuatia kupata majeraha katika mkono wake wakati wa Kombe la Mapinduzi Cup hali iliyopelekea kufungwa hogo.
FIT KUREJEA KIKOSINI : Good News ni kwamba mchezaji wetu Dany Usengimana ameshaondolewa “hogo” kwenye mkono wake, tayari ameshakamilisha matibabu yake na anaungana na wachezaji wenzake hivi karibuni.
@danny_usengimana alipata majeraha ya mkono wakati wa michuano ya Mapinduzi Cup na kumuweka nje ya uwanja kwa wiki tatu.
Singida ipo nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kwakuwa na alama 27 wakati ya tatu ikishikwa na Yanga SC yenye pointi 28 huku ya pili ikiwa Azam FC yenye 30 huku vinara Simba SC wakiwa na 35.
Post A Comment: