Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai alikuwa akitoka kimapenzi na Young Dee.
Rosa Ree amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani yeye na Young Dee walikuwa pamoja kwa ajili ya kazi tu.
“Mimi na Young Dee tulienda kufanya tour pamoja, tulienda kufanya kazi. Katika industry yetu, society yetu ni kama ukimuona mtu ana come together na mtu mwingine unachukulia wanatoka pamoja, hapana haiko hivyo,” Rosa Ree Alisema
“Labda inaweza ikawa hivyo kwa watu wengine haikuwa hivyo iliishia kwenye kazi, mimi na Young Dee hatuna mahusiano wa kimapenzi,” amesema.
Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Marathon’ aliyomshirikisha Bill Nass mara baada ya kutamba na ngoma ‘Dow’.
Post A Comment: