John Bocco
Klabu ya Simba huenda ikawatoa kimasomaso Watanzania kwenye michuano mikubwa barani Afrika ya Kombe la Shirikisho kutokana na ushindi mnono wa leo wa goli 4-0 dhidi ya klabu ya Gendamarie Tnale kutoka nchini Djibouti.
Magoli ya Simba yamefungwa na John Bocco 33′, 44′ , Emannuel Okwi 90+ na Said Ndemla kunako dakika ya 2 ya mchezo.
Kwa ushindi huo hakuna shaka kuwa Simba watafanikiwa kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano hii ni kwa jinsi kikosi cha Gendamarie Tnale kilivyo hakitakuwa na uwezo wa kumtwanga mnyama goli 5-0 ili kusonga mbele ingawaje mpira haupo hivyo ila Simba wameonesha matumaini kwa Watanzania.
Hayo yamejiri wakati ambapo mahasimu wao Klabu ya Yanga jana wamepata ushindi  mwembamba wa goli 1-0  dhidi ya St Louis mchezo wa klabu bingwa Afrika raundi ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: