Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA) Salum Mwalimu amesema biashara ya kuvunjiwa nyumba wananchi wa jimbo hilo imefika mwisho kwa madai yeye binafsi hofu na adhabu ya kuvunjiwa anaifahamu kwa maana anaishi maeneo hayo.
Salum Mwalimu ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni ambapo kwa sasa zimebakia takribani siku 13 kuingia katika chaguzi ndogo za kumtafuta Mbunge wanayemtaka katika Jimbo lao ambalo kwa sasa lipo wazi.
"Hofu na adhabu ya kuvunjiwa nyumba ninaijua kwa sababu na mimi nipo pembezoni mwa bonde hivyo wakiendelea na bomoa bomoa maana yake na mimi itanikumba. Kwa hiyo adha hiyo hawezi kutoka mtu mwingine wa mbali aje kuizungumzia, mimi ninaijua", alisema Salum Mwalimu.
Pamoja na hayo, Salum Mwalimu aliendelea kusisitizia kwamba "ninataka niwaambie ndugu zangu, labda masela mnikimbie lakini kama washkaji na masela tutazungumza lugha moja biashara ya mtu kuvunjiwa nyumba yake sio Hananasif tu, bali ndani ya Jimbo la Kinondoni bila ya utaratibu au kutangulizwa kwanza fidia biashara hiyo inaenda kukoma ninawaapia hilo".
Kwa upande mwingine, Mama wa mgombea huyo ambae alijitambulisha kwa jina la Faudhat Abood katika kampeni hizo amewaomba wananchi wa jimbo la Kinondoni wasisikilize maneno ya watu yanayodai kuwa Salum Mwalimu sio mtu wa Dar es Salaam.
Post A Comment: