Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) umesema kuanzia sasa Watanzania ni ruksa  kutumia Kitambulisho cha Taifa na kile cha kupiga kura kupata cheti cha kuzaliwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 8, 2018 na kaimu ofisa mtendaji wa Rita, Emmy Husdon wakati akitoa taarifa kwa katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome aliyefanya ziara katika ofisi za Rita, jijini Dar es Salaam.

"Vyeti vya vizazi na vifo vinaweza kutolewa papo kwa hapo katika hospitali na vituo vya afya vilivyo katika majaribio,” amesema Husdon na kuongeza:

“Vituo hivyo ni pamoja na Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Mbagala Rangitatu, Mbande Dispensary, Mnazi Mmoja, Kairuki na Hospitali ya Kinondoni.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: