MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya maamuzi magumu kwa viongozi wa mkoa wake baada ya kusimamisha shughuli zote za mabaraza ya kata kwa wilaya zote mkoani humo pamoja na kesi zote hadi uataratibu wa kupitia upya taaluma za wanasheria wa mabaraza hayo utakapofanyika.

Makonda amefanya maamuzi hayo leo feb. 10, 2018 wakati akitatua kero za wananchi wa Dar es Salaam alipokuwa akifanya mkutano nao katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar na kuwataka makatibu tarafa kuanza kutembelea mabaraza hayo kuanzia Jumatatu ili kuziainisha kesi hizo na kuanza kuzitatua.

RC Makonda amewasimamisha kazi wakuu wa Idara za mipango miji manispaa ya Ilala na Ubungo kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

“Kuanzia Jumatatu nataka wakurugenzi muniletee CV zote za wakuu wenu wa Idara kwa sababu matatizo ya wananchi ni mengi lakini sioni kazi yao wanayofanya.

“Hawa wakuu wa idara wanalipwa mishahara, posho, wanapewa nyumba, wanapewa pesa za mawasiliano vyote hivyo, lakini hakuna wanachokifanya, kwa nini?

“Kinatukanwa CCM kwa uzembe wa mtu mmoja amekaa kwenye kiti ofisini anakula tu, ni sawa na kulipa mshahara kwa watumishi hewa. Wakurugenzi naomba mjitathmini, tunasoma ripoti zenu nzuri tukipita mtaani wananchi wanatushangaa,” alisema Makonda.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: