Leo Jumapili February 4, 2018 Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara inaendelea baada michezo 5 Kuchezwa jana katika Viwanja Mbali Mbali nchini Tanzania.
Michezo ya Leo
Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kutakuwa na mchezo kati ya Wenyeji wa Mchezo wa Leo Timu ya Stand United (Chama la wana) dhidi ya wana TamTam Mtibwa Sugar waliosafiri kutoka Manungu Turiani
Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Katika uwanja wa Kirumba Jijini Mwanza kutakuwa na Mchezo kati ya Mbao Fc wanaodhaminiwa na Kampuni ya GF Trucks wakiikaribisha Kagera Sugar (Wanankurukumbi) waliosafiri kutoka Mkoani Kagera mpaka jijini Mwanza Kuwafata Mbao Fc.
Uwanja wa Uhuru
Katika dimba la Uhuru Kutakuwa na Mchezo kati ya Ruvu Shooting watoto wa Masau Bwire wakiwa wenyeji wa Simba ambao wanatokea katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar Es Salaam.
Ruvu msomaji wa Kwataunit Wanakumbuka Kichapo cha Bao 7 kwa 0 walichokipata katika Mchezo wa awali kutoka kwa Simba raundi ya Kwanza.
Matokeo mechi za JANA
Singida United 3 – 2 Mwadui
Maji Maji 1 – 2 Mbeya City
Prisons 2 – 0 Njombe Mji
Azam 3 – 1 Ndanda.
Post A Comment: