Kikosi cha Mtibwa Sugar weekend hii wanataraji kushuka uwanjani kukipiga dhidi ya Stand United ya Shinyanga katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League)  uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga 
Mchezo huo wa ligi kuu bara unatarajiwa kuchezwa saa 8 mchana siku ya Jumapili, awali mchezo huo ulikuwa uchezwe siku ya Jumamosi lakini ratiba ilibadilishwa kutokana na maombi ya Mtibwa Sugar kuomba mchezo huo upelekwe siku ya Jumapili.
Sababu ya wana tam tam  kuomba mabadiliko hayo ya ratiba ni kutokana na safari ndefu ya kutoka Lindi walipokuwa wameenda kucheza mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Maji Maji Rangers ambao wana tam tam wali ibuka na ushindi wa goli 1-2, safari hiyo inawalazimu wana tam tam kufika mkoani Shinyanga siku ya Ijumaa na siku ya Jumamosi ambayo ilikuwa siku ya mchezo wenyewe wanaitumia kwa mapumziko na hivyo mchezo huo wa raundi ya 16 unatarajiwa kuchezwa Jumapili saa 8:00 mchana.
Mabingwa wa ligi kuu bara wanaoneka kuwa bora na kuimalika zaidi msimu huu baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 26 katika michezo 15 ya ligi kuu bara huku wapinzani wao wakifanikiwa kukusanya pointi 13 katika michezo 15 ya ligi kuu bara.
Kikosi cha wana tam tam kipo kamili na wachezaji wote woko katika hali nzuri ya kuendelea kupambana isipokuwa Riphat Khamis aliyeumia katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: