Kufuatia kifo cha msanii wa muziki Radio aliyefariki alfajiri ya leo nchini humo, Rais wa Uganda Yoweri Museven ameonyesha hisia zake kwa kuguswa na kifo cha msanii huyo.
Kupitia  mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Museven ameandika “Have been told about the untimely death of musician Moses Ssekibogo aka Mowzey Radio. I had only recently made a financial contribution towards his treatment and hoped he would get better. He was a talented young person with a great future ahead of him. May he rest in peace.”
Taarifa za kifo cha msanii huyo zinakuja baada ya  siku chache zilizopita Rais Museven kutoa kiasi cha  Milioni 30 kwa ajili ya  matibabu ya msanii huyo.
Vile vile wasanii mbalimbali kama Navio, Diamond, Eddy Kenzo, Professa Jay  na wengineo wametumia kurasa zao   za mitandao yao ya kijamii kama Instagram na Twitter kutoa pole kwa familia yake.
Baada ya kutangazwa taarifa za kifo mashabiki wa msanii huyo na wa Goodkife walifika hospitali hapo kushuhudia kinachoendelea.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: