Rais wa Jamhuri y aMuungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaji Mlemavu wa viungo Bw. Yusuf Abdulrahaman Ndemanga.
Bw. Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw.Ngusa Samike, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Februari, 2018.
Mhe. Rais Magufuli alikutana na Bw. Ndemanga tarehe 25 Agosti, 2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na Mhe. Rais Magufuli, Bw. Ndemanga alimuomba msaada wa kupatiwa Bajaj ili imsadie kupata kipato.
Akikabidhi msaada huo Bw. Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri na kujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.
“Mhe. Rais amenituma nikukabidhi Bajaj hii mpya kabisa, matarajio yake ni kuwa itakusaidia kupiga hatua za kimaendeleo, anatarajia kukuona unaongeza Bajaj nyingine na unaisaidia familia yako kupata nafuu ya maisha na sio kuja kuomba msaada mwingine”amesema Bw. NgusaSamike.
Kwa upande wake Bw. Ndemanga aliyeongoza na Mkewe Bi. Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa wataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwaajili ya familia yake.
“Naomba mkamwambie Mhe. Rais kuwa namshukuru sana, na namuombea dua Mwenyezi Mungu amlinde na kumzidishia hekima na upendo kwetu sisi wananchi hasa sisi walemavu”amesema Bw. Ndemanga.
Post A Comment: