Mapema siku ya leo Jumapili Februari 25, 2018, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.  Joyce Ndalichako amewashukia watumishi wa umma wenye ajira mbili na kuwataka kujiuzulu moja ya ajira kati ya hizo mbili, na kubakia na ajira moja pekee.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Arusha alipotembelea katikia Chuo Kikuu cha Mount Meru ili kujionea miundombinu na namna wanavyosimamia suala la utoaji elimu ya juu chuoni hapo.
Akiwa chuoni hapo, Prof. Ndalichako ameonesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watumishi wa umma kuwa na ajira mbili kwa wakati mmoja, wakifanya serikalini na kwenye taasisi binafsi kwa mkataba kamili (full time) na hivyo kuwataka kuacha kufanya ivyo mara moja.
Kauli hiyo ya Ndalichako inafuatia kugundua kuwa baadhi ya wafanyakazi katika chuo hicho ni waajiriwa wa serikali na hivyo kupokea mishahara miwili kwa wakati mmoja, yaani ule wa serikali na wa taasisi binafsi.
“Kanuni za utumishi, kifungu cha F cha namba 4 na 7, kinazuia mtumishi wa umma kuwa na ajira mbili, na mtumishi wa umma akiwa na ajira mbili, automatically anapoteza ajira yake kwenye utumishi wa umma” amesema waziri Ndalichako
Katika htua nyingine waziri Ndalichako ameonesha kukerwa na upikaji wa alama unaofanywa na baadhi ya wahadhiri wasiokuwa waaminifu, na wazalendo kwa taifa, na hivyo kuwataka kuacha kufanya vitendo vya namna hiyo mara moja iwezekanavyo.
“Suala la kupika alama za wanafunzi, ni suala ambalo Tanzania hatujafika hapa” amesema Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako amehitimisha ziara yake chuoni hapo kwa kuutaka uongozi wa chuo kuwaondoa wahadhiri wote wasio na sifa za kufundisha chuoni hapo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: