POLISI Wilaya ya Kinondoni imesema itapambana na watakaovuruga uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu. Pia imesema maiti aliyeokotwa katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ni mwanachama wa chama gani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro, amesema jukumu lake ni kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
Pia ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa bila kuleta vurugu.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema lilipokea habari kutoka kituo cha polisi cha Oyster Bay ambako msamaria mwema aliripoti kuokotwa kwa maiti ya mtu mmoja katika ufukwe wa Coco Beach wa Bahari ya Hindi.
“Jeshi la polisi liliwatuma askari kwenda eneo la tukio na kukuta mwili wa mtu mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mika 30-35 ukiwa na majeraha mengi mwilini ambapo ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo madaktari walibaini kuwa amekwishafariki,” alisema .
Mmoja waandishi wa habari alipouliza kuhusiana na mtu huyo kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kama ilivyodaiwa kuripotiwa na chamahicho, Muliro alisema kuwa hana taarifa ya chama cha marehemu huyo.
Post A Comment: