Polisi wa huko jijini Seville nchini Hispania wakamata watu watano jana baada ya kufukuzana nao kwa kasi na ndipo hapo polisi waligundua tani hizo za machungwa zilizoibiwa ambazo watuhumiwa walikuwa wameyajaza ndani ya magari.
polisi walipatwa na shaka wakati walipoona magari matatu yakikunja kona ya haraka kutokana na Ripoti ya Europa Press. Baada ya kukimbizana nao, polisi waliweza kusimamisha magari mawili. Walipofungua mlango wa nyuma wa gari mamia ya machungwa yalidondoka chini.
Machungwa hayo yalirudishwa katika mji wa Carmona, ambayo ndiyo mji uliotoa ripoti za wizi masaa machache tu kabla ya tukio hilo.
Polisi walisema kuwa karibu poundi 9,000 za matunda yalipatikana na uchunguzi wa wizi unaendelea.
Post A Comment: