Ni jambo la kawaida kwa msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz kuonekana akila bata la nguvu katika nchi zilizoendelea.
Siku ya jana Ommy Dimpoz alikuwepo nchini Uingereza ambapo alishuhudia mchezo kati ya Manchester United na Tottenham Hotspurs uliopigwa kwenye uwanja wa Wimbley. Mchezo huo ulimalizika kwa Tottenham kushinda 2-0.
Katika matembezi yake Uingereza Ommy Dimpoz amekutana na mchezaji kutoka nchini Kenya, Victor Wanyama ambaye anaichezea Tottenham.
Utakumbuka July mwaka 2016 Ommy Dimpoz alikutana na Wayne Rooney nchini Uhispania katika kisiwa cha Ibiza ambapo alikuwepo na familia yake kwa mapumziko. Kipindi hicho Wayne Rooney alikuwa akikipiga katika timu ya Manchester United kabla ya kujiunga na Everton.
Post A Comment: