Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chama cha Demookrasia na Maendeleo-CHADEMA ambaye hivi karibuni alikihama chama hicho na kuhamia CCM Patrobas Katambi amejitokeza kwa mara ya kwanza na kueleza udhaifu mkubwa wa kiuongozi uliopo ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Patrobas amesema, vyama vingi vya siasa vya upinzani vimekuwa mali ya wenyeviti wa vyama hivyo na kueleza kuwa haviwezi kusonga mbele kutokana na mwenendo wa vyama hivyo.
Katambi amesema kuwa vyama vya siasa vya upinzani, vimekuwa vikifuja fedha za ruzuku na mara zote vimekuwa vikipata hati chafu katika matumizi yao ya ruzuku na fedha nyingine za chama.
Mwanasiasa huyo machachari amesema, alimua kutoka-CHADEMA kutokana na kupotea kwa ajenda na hoja za msingi na kusema kuwa wote waliobakia katika vyama vya upinzani wananufaika na mfumo uliopo.
Post A Comment: