Muigazaji wa filamu na mchekeshaji nchini Tanzania Idris Sultan amefunguka na kudai abarikiwa kupendwa zaidi na watu wengi hasa wanawake japo kuwa yeye sio mwanamuziki
Idris amebainisha hay alipokuwa akijibu swali la mwandishi aliyetaka kufahamu kwamba kama aliweza kuwa katika mahusiano mengine baada ya kuachana na Wema Sepetu.
"Hapana sijawahi lakini yapo majaribio ya mpito, nilikuwa 'single' kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu (miezi 18), siwezi kuhesabu mahusiano ya mara ya mwisho nilikuwa wiki moja sijui yule msichana alikuwa na shida gani", amesema Idris.
Pamoja na hayo, Idris ameendelea kwa kusema "unajua wanaume tunaogopa kusema ukweli lakini inatubidi tuongee ukweli tu. Kwa nafasi niliyokuwa nayo mimi nimezungukwa sana na 'a lot of fans' kwa mtu ambaye sio mwanamuziki, sio msichana nahisi kama nimebarikiwa sana kupendwa na watu.
'I think' mimi ni mtu pekee ambaye sio mwanamuziki wala msichana mwenye 'following' kubwa kiasi hicho na nipo katika kiengo changu mwenyewe najua nafanya nini, basi tu na watu wangu mimi nawapenda kama wanavyonipenda".
Kwa upande mwingine, Idris amedai sababu kubwa za kutostawi kwa penzi lake hilo jipya ni kutokana na mrembo huyo kuhofia kuumizwa moyo wake kutokana mchekashaji huyo kupendwa sana na mashabiki zake.
Mtazame hapa chini Idris Sultan akiendelea kufunguka kuhusiana na mahusiano yake aliyoyapitia mpaka kufikia leo hii.
Post A Comment: