MKONGWE wa filamu za Kibongo aliye kipenzi cha wengi, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ambaye kwa sasa ni mgonjwa ametoa ya moyoni kuwa bado anaumwa hivyo kuwaomba wasanii wenzake na Watanzania kumuombea.
Akizungumza na Star Mix, Mzee Majuto alisema Februari 11, mwaka huu anatarajia kurudi tena katika Hospitali ya Tumaini, Dar alikokuwa amelazwa awali na kuruhusiwa baada ya daktari wake kufiwa ambapo ndiyo ataenda kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume unaomsumbua.
“Niliruhusiwa Jumamosi iliyopita lakini bado naumwa, tezi dume si mchezo, ninachoweza kuwaambia wasanii wenzangu na Watanzania kwa jumla, waniombee tu,” alisema Mzee Majuto.
Post A Comment: