Muigizaji King Majuto ameruhusiwa Hospitali  jana Jumamosi kwa ajili ya kwenda kujitazamia nyumbani kwa muda.
Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Masoud kaftany ilisema, muigizaji huyo nguli, Alhaji Amri Athuman ‘King Majuto’ jana Jumamosi  amepewa ruhusa kwenda nyumbani na kapangiwa siku ya kurudi  tena Hospitali ya Tumaini  tarehe 11/2/2018.
King Majuto alilazwa wiki moja katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: