Amesema miaka ya nyuma wakati utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo haujaanza, baadhi ya raia wa kigeni walikuwa wakitumia mwanya huo kunufaika na huduma za jamii kama elimu.
“Watu hao walipomaliza masomo walirejea katika nchi zao na kuzinufaisha kwa namna moja au nyingine wakati wametumia pesa za watanzania. Mnapaswa kuwa makini ili kubaini wageni,” amesema Mwigulu.
Amesema kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuhakikisha hakuna mgeni anayepenya na kupata kitambulisho hicho.
“Uandikishaji na utoaji wa vitambulisho hivi ni bure. Wananchi hawapaswi kutozwa fedha yoyote,” amesema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Massawe amesema lengo ni kuhakikisha mpaka Desemba, 2018 utoaji wa vitambulisho hivyo uwe umefanyika nchi nzima.
Ametaja faida za vitambulisho hivyo kuwa ni kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na wananchi kutambulika haraka wanapokwenda kupata huduma mbalimbali, zikiwemo afya na elimu.
Post A Comment: