Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Meru mkoani Arusha Mh Simoni kaaya,ametoa tamko lakushushwa vyeo kwa walimu wakuu ambao shule zao zitaendelea kufanya vibaya ili kuweza kuboresha elimu kwa wanafunzi.

 Akizungumza katika ziara yake aliyofanya katika kata ya Leguruki,Wilayani Meru,ametoa tamko hilo kwakumwambia mkurugenzi na afisa elimu wilaya kuwa shule zote zitakazo endelea kufanya vibaya,walimu wa shule hizo washushwe vyeo na nafasi zao kupatiwa waalimu wenye uwezo na ubunifu.


Aidha Mh Simoni Kaaya amesema kauli ya Mh. Rais Magufuli ya Tanzania ya viwanda inajumuisha Mashine na watu,hivyo nilazima kukazia swala la elimu,mazingira na malezi ili kuweza kupata nguvu kazi yakufanya kazi katika viwanda.


 Hata hivyo Simoni amelisemea swala la waratibu wa kata kutotembelea shule zao,nakusema mamlaka waliyopewa  kwakuteuliwa kuwa waratibu wanapaswa kufanya kazi kama inavyopaswa na sivyo kama baadhi yao wafanyavyo.


Pia mwenyekiti huyo amewataka wakuu wa shule na wakazi meru kuhakikisha wanaendelea kuboresha mazingira kwa kupanda miti sambamba na kuboresha kutunza na kuvilinda  vyanzo vya maji  kwa ajili ya vizazi vijazo.

Mh Simon amefurahishwa na utendaji kazi wa Katibu Tawala Meru Mh: Timoth Mzava na mkurugenzi wa Meru Bwana Christopher J. Kazeri na kuwapongeza kwa kupokea kero na changamoto anazowapelekea kutokana na Ziara zake na kuzitatua kwa wakati.
Share To:

Post A Comment: