Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi ameapishwa rasmi leo Bungeni, Mjini Dodoma.
Mara baada ya kula kiapo cha uaminifu, AG amekabidhiwa vitendea kazi na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.
Utakumbuka Februari Mosi mwaka huu ndipo Rais Magufuli alimteua Dkt. Kilangi kuwaMwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu. Wakati huo huo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Dk Kilangi ameapa leo kabla ya kuanza kwa kikao cha tano cha mkutano wa 11 wa Bunge, mjini Dodoma.
Post A Comment: