Na Mwandishi Wetu, Kinondoni
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Maulid Said Mtulia anatarajia kuunguruma leo Jumatano Februari 7, 2018 katika kata viwanja vya Vegas, kata ya Makumbusho.
Huu ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni inayoendelea kufanyika kata mbalimbali mgeni rasmi wa leo akitarajiwa kuwa Mhe. Livingstone Lusinde.
Watu wengi sana hujitokeza kwenye mikutano yake ya kampeni. Akizungumza juu ya mikutano hiyo, mkaazi wa Kinondoni Godfrey Baraka amesema Mtulia ameonyesha utofauti na wagombea wenzake kwa kunadi zaidi sera kuliko matusi, kebehi na ushabiki ndio maana mikutano yake hufurika Watu wa kada tofauti tofauti.
"Ukienda kwenye mikutano ya Mtulia utasikia akinadi ilani ya uchaguzi ya CCM. Utasikia Mtulia akieleza namna atajenga miundombinu, ataboresha huduma za kijamii, namna atakavyo wawezesha kiuchumi Vijana na Wanawake. Ni tofauti kabisa na wagombea wengine ambao wao kutwa kutukana, ushabiki na kebehi tu" alisema Godfrey.
Akizungumza juu ya Mkutano wa kampeni wa leo Katibu CCM wilaya ya Kinondoni amewasisitizia wakazi wa Kata ya Makumbusho na viunga vyake pamoja na wakazi wote wa jimbo la Kinondoni kuwahi mapema mkutanoni.
"Nawasisitiza Wanachama CCM na Wananchi wote kwa ujumla kuwahi mapema katika Viwanja vya Vegas Kata ya Makumbusho waje wasikilize kipi Mtulia anawahaidi kuwafanyia, waje wamsikilize mgeni rasmi
Mhe Lusinde almaarufu Kibajaji na sera anazokuja kuwaambia wana Kinondoni." alisema Katibu.
Mkutano wa leo unatarajia kuanza majira ya saa 8 mchana katika viwanja vya Vegas, Kata ya Makumbusho.
Post A Comment: