Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka na kumtetea mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania ambaye sasa anakipiga klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji , Mbwana Samatta kuwa ameshinda kwenda kumtembelea Tundu Lissu kutokana na ratiba yake kuwa ngumu.

Zitto Kabwe aliona aweke wazi hilo kufuatia baadhi ya watu kuanza kuhoji inakuaje mchezaji huyo yupo ameshinda japo kwenda kumtembelea na kumuona Mbunge Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini humo kufuatia kushambuliwa kwa risasi mwaka jana. Zitto Kabwe ndipo aliamua kuweka sawa kuwa mchezaji huyo kwa sasa ratiba yake ni ngumu lakini anaamini atakwenda wakati ukipatiakana.

"Mbwana ni mgonjwa pia. Hivi sasa yupo kwenye mazoezi chini ya ratiba ngumu Sana ili arudi hali yake ya kawaida. Mjue kuwa Mbwana ni profeshno hawezi kwenda kinyume na ratiba ya daktari kama huko kwetu. Msimwingize kwenye haya mambo tafadhali. Atamwona Lissu kwa wakati wake" aliandika Zitto Kabwe 

Zitto Kabwe kwa sasa yupo nchini Ubelgiji ambapo alipata nafasi ya kumtembelea Mbunge Tundu Lissu anapopatiwa matibabu pia aliweza kumtembelea mchezaji huyo wa Genk
Share To:

msumbanews

Post A Comment: